Connect with us

Riadha

Tanzania Yaburuza Mkia Riadha

Timu ya riadha kutoka Tanzania imefanya vibaya katika mashindano ya riadha Afrika yanayoendelea nchini Morocco baada ya wanariadha watatu kushika nafasi ya mwisho katika mashindano hayo.

Wanariadha hao  Ally Gulami, Benjamin Kulwa na Regina Mpigachai wameshindwa kutamba katika mbio hizo baada ya Ally Gulami kutumia sekunde 48.96 na Benjamini kula kutumia sekende 50.85 katika mbio za mita 400 huku Regina Mpigachai akitumia sekunde 2.13 mita 800.

Matokeo hayo ni pigo kwa Timu za Tanzania katika michezo hiyo ya 12, inayofanyika jijjni Rabat baada ya Judo kuondoshwa katika hatua za awali ikiwa ni siku 1 tu kabla ya hafla ya ufunguzi Agosti 19.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Riadha