Connect with us

Other Sports

Shakira,Pique Watengana

Mastaa Gerrad Pique wa Fc Barcelona na mke wake Shakira sabel Mebarak Ripol wametengana baada ya kuwa katika mahusiano kwa miaka 11 ambapo wamefanikiwa kupata watoto wawili Nilan na Sasha.

Mastaa hao ambao mahusiano yao yalianza wakati wa fainali za kombe la Dunia nchini Afrika ya kusini wamedaiwa kutengana huku sababu kubwa ikiwa ni Pique kukutwa na kashfa ya usaliti katika ndoa yao na tangu hapo wamekuwa wakiishi tofauti baada ya Pique kufukuzwa katika nyumba ya familia,kwa mujibu wa jarida la Hispania El Periodico.

Shakira mwenye umri wa miaka 45 akiwa amempita Pique miaka 10 alichapisha taarifa akielezea chanzo cha kuachana kwao ‘Tunajuta kuthibitisha kwamba tunaachana. Kwa ajili ya ustawi wa watoto wetu, ambao ni kipaumbele chetu cha juu, tunaomba uheshimu faragha yao. Asante kwa kuelewa kwako.’

Hii ilikua ni moja ya safu ya wapenzi iliyokua ikipendwa sana na mashabiki wa soka duniani pamoja na zile za wakina Cristiano Ronaldo na Lionell Messi kutokana na ustaa wa wahusika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Other Sports