Connect with us

Makala

Che Malone Kuikosa Al Masry

Beki wa klabu ya Simba Sc Che Malone Fondoh anatarajiwa kuukosa mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Aprili 2 2025.

Beki huyo aliumia katika sare ya 2-2 dhidi ya Klabu ya Azam Fc ambapo mpaka sasa bado hajarejea uwanjani licha ya juhudi kubwa za matabibu wa klabu hiyo.

Mabosi wa klabu hiyo walimpeleka nchini Morocco kwa ajili ya matibabu lakini mpaka sasa bado hajapona vizuri kiasi cha kucheza michezo migumu.

“Taarifa kuhusu mchezaji wetu Che Malone ni kwamba yupo nchini Morocco anaendelea na matibabu na baadaye madaktari wetu watatupa taarifa kwamba ni lini mchezaji wetu huyu atarudi uwanjani kuendelea na majukumu yyake.Alisema Ahmed Ally meneja wa idara ya habari ya klabu hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Simba sc inatarajiwa kuondoka nchini Machi 28 kuanza safari ya kuelekea nchini misri kwa ajili ya mchezo wa duru la kwanza April 2 2025.

 

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala