Connect with us

Masumbwi

W/Mkuu: Tunasubiri Mwakinyo vs Kiduku

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kuwa anasubiria kwa hamu pambano la mabondia wawili wanaofanya vizuri nchini Twaha kiduku na Hassan Mwakinyo.

Majaliwa ameyasema hayo wakati wa kufunga vikao vya bunge jijini Dodoma.Wazri mkuu katika hotuma yake hiyo aliwapongeza mabondia hayo kwa ushindi katika mapambano yao yaliyofanyika hivi karibuni.

Mh Majaliwa alisema ”ninawapongeza sana mabondia wetu Twaha Kiduku kwa kumtwanga Dulla Mbabe katika pambano lililovuta hisia za Watanzania wengi,laini vilevile nimpongeze sana bondia wetu Hassan Mwakinyo lwa kumdunda mpinzani wake Mnamibia Julius Indongo kwa knockout”.

Aliendelea kwa kusema ”wanamasumbwi wetu wameifanya Tanzania itambulike zaidi ulimwenguni,sasa Watanzania tunasubiri pambano la watani kati ya Mwakinyo na Kiduku,hatujui ni lini litatokea”.

Kauli hiyo imeonesha kuwa si wadau wa ngumi pekee wanaolitaka pambano hilo bali pia hata viongozi wa serikali na Watanzania wote kwa ujumla kumaliza ubishi ni nani bondia bora bora zaidi  hapa Tanzania.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi