Connect with us

Makala

Yao Kouasi Nje Wiki Sita

Mlinzi wa Kulia klabu ya Yanga Sc Yao Kouassi Attouhoula atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne mpaka sita akiuguza majeraha ambayo yanamkabili.

Yao anasumbuliwa na matatizo ya mguu wake wa kulia hali ambayo imemfanya kukosa michezo kadhaa ya ligi kuu na michuano ya Kimataif.

Meneja wa habari na mawasiliano wa Young Africans,Ali Kamwe amethibitisha hilo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Mc Algers siku ya Januari 18 mwaka huu.

“Mchezaji wetu Yao Kouasi Attouhoula hatakuwa sehemu ya kikosi baada ya kufanyiwa upasuaji na atakuwa nje kwa kipindi kisichopungua wiki nne na kisichozidi wiki sita”,Alisema Kamwe.

“Maxi Nzengeli anaendelea vizuri na maozezi, kama mwalimu ataona utimamu wake wa kimwili unafaa kucheza mchezo ujao basi atamtumia lakini kimsingi kwa sasa yupo salama”,Alimalizia kusema Kamwe kwa msisitizo.

Yanga sc itakua na mchezo mgumu dhidi ya Mc Algers siku ya Jumamosi Januari 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mchezo huo utaamua hatma ya klabu hiyo kama itafuzu robo fainali ama la.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala