Connect with us

Makala

Yanga sc,Saido Wafikia Mwisho

Klabu ya Yanga sc imeachana na mshambuliaji Saido Ntibanzokiza baada ya mkataba wake kufikia ukingoni hivi leo na klabu hiyo kuamua kutoa taarifa rasmi kuhusu kuachana huko.

Saido alijiunga na Yanga sc kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa kama mchezaji huru baada ya kutokua na timu ambapo Yanga sc ilimuona alipokua akiichezea timu ya taifa ya Burundi ilipokua ikicheza na Taifa Stars jijini Dar es salaam.

Inasemekana kwamba Yanga sc ilikua na mpango wa kumuongezea staa huyo mkataba wa mwaka mmoja lakini staa huyo alitaka miaka miwili huku pia licha ya kuwa na kiwango kizuri staa huyo amekua na matatizo ya kinidhamu hasa baada ya kutoroka kambini walipokua wakijiandaa na mchezo dhidi ya Simba sc ambapo kocha Nabi alimua kuwasimamisha yeye na Dickson Ambundo ambapo walitakiwa kurudi jijini Dar es salaam.

Taarifa zinadai staa huyo badala ya kurudi Dar es salaam yeye aliamua kwenda nyumbani kwao Burundi bila kuaga huku akigoma kusubili kikao cha maamuzi kilichopangwa kufanyika leo jijini Dar es salaam ndipo klabu hiyo ilipoamua kuachana nae.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala