Connect with us

Makala

Yanga Sc,Azam Fc Kucheza Caf Champions League

Baada ya kutamatika kwa pazia la ligi kuu nchini ambapo jumla ya michezo 30 imemalizika kwa timu zote 16 za ligi kuu na klabu ya Yanga sc kumaliza kuwa mabingwa wa ligi hiyo wakifikisha alama 80 huku Azam Fc ikishika nafasi ya pili ikikusanya alama 69 sambamba na Simba sc iliyoshika nafasi ya tatu ikizidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Baada ya ligi kumalizika sasa tayari imefahamika kuwa Yanga sc na Azam Fc moja kwa moja zitakwenda kushiriki michuano ya kimataifa ya kombe la klabu bingwa barani Afrika ambalo ndio kombe kubwa kwa sasa sambamba na lile la African Football league huku Simba sc na Coastal Union zenyewe zikikata tiketi za kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limeonyesha nia ya kuifuta michuano hiyo ya kombe la Shirikisho kutokana na ujio wa michuano ya kombe la African Football league ambalo linaziingizia vilabu fedha nyingi kuliko michuano yeyote barani Afrika lakini mpaka sasa taarifa rasmi ya kuifuta michuano hiyo bado haijatoka na kufanya vilabu vijiandae na michuano hiyo.

Simba Sc na Yanga Sc kama michuano ya kombe la Shirikisho haitafutwa basi zitakua na faida ya kuchaguliwa kushiriki michuano ya kombe la Super League kutokana na msimu ujao michuano hiyo itashirikisha vilabu 24 ambavyo vina alama nyingi katika michuano hiyo kitu ambacho vilabu hivyo vinafuzu moja kwa moja.

Msimamo wa ligi kuu umetamatika kwa Simba sc kushinda 2-0 dhidi ya Jkt Tanzania huku Yanga sc ikishinda 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons na Azam Fc yenyewe imeshinda 2-0 huku timu za Geita Gold Fc na Mtibwa Sugar zikishuka daraja moja kwa moja na klabu za Tabora United na Jkt Tanzania zikilazimika kutetea nafasi zao katika michezo ya “Play Off” ili kujua hatma yake ambapo zitacheza na timu za ligi daraja la kwanz  maarufu kama “Championship” ambapo mshindi ndio atafuzu kwenda ligi kuu msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala