Connect with us

Makala

Yanga Sc Yazidi Kujichimbia kileleni

Klabu ya Yanga sc imezidi kujichimbia katika kilele cha msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga klabu ya Singida Black Stars kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.

Yanga sc ikianza na kasi yake ya kila siku ilifanikiwa kupata mabao mawili ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Clement Mzize dakika ya 13 na Prince Dube dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza huku Singida Black Stars wakipata bao la dakika za mwishoni kupitia kwa Jonathan Sowah dakika ya 90+2.

Mzize alifunga bao la kumi kwake kwa shuti kali baada ya kuamua kupambana na mabeki kuuwahi mpira uliokua unazagaa ndani ya boxi.

Yanga sc ilikosa nafasi kadhaa lakini Dube alifanikiwa kuruka juu na kuwazidi maarifa walinzi wa Black Stars na kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Maxi Nzengeli.

Kocha David Ouma wa Singida Black Stars ni kama alitaka kifungwa baada ya kuwaanzisha mabeki ambao hawajazoeana akiwemo Morice Chukwu ambaye alichezeshwa kama mlinzi wa kati badala ya kiungo kama ilivyozoeleka huku akiwaacha nje mastaa kama Anthony Bi Tra Bi,Kennedy Juma,Athur Bada na Jonathan Sowah ambao baada ya kuingia waliibadili mechi.

Yanga sc sasa imefikisha alama 52 katika nafasi ya kwanza ikicheza michezo 20 ya ligi kuu huku Singida Black Stars ikisalia katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu na alama 37 ikicheza michezo 20 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala