Connect with us

Makala

Yanga sc Yawasili Singida

Msafara wa klabu ya Yanga sc umewasili salama mkoani Singida kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida Black Stars siku ya kesho jumatatu machi 24.

Yanga sc inatarajiwa kumemyana na klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya sherehe za kufungua uwanja mpya wa klabu ya Singida Black Stars unaoitwa Airtel stadium.

Katika msafara huo mastaa wa Yanga Sc ambao hawajaitwa timu za taifa wamesafiri na Timu akiwemo Stephan Aziz Ki,Bakari Mwamnyeto na Pacome Zouzoua.

Wengine ni Kibwana Shomari,Nickson Kibabage,Shadrack Boka,Maxi Nzengeli,Prince Dube sambamba na AbouTwalib Mshery,Abubakar Salum na Aboubakari Khomeini.

Mchezo unatarajiwa kuvutia mashabiki wengi mkoani humo kutokana na vikosi vya timu zote kujaa mastaa wa maana.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana Yanga sc iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala