Connect with us

Makala

Yanga Sc yawasili Mwanza Kibabe

Msafara wa kikosi cha timu ya Yanga sc umewasili salama jijini Mwanza kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Pamba Jiji utakaofanyika siku ya Jumamosi Februari 28 katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Kikosi cha mastaa wa klabu hiyo kiliwasili uwanja wa ndege mapema Februari 26 na kupokelewa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo waliofurika kuanzia uwanja wa ndege jijini humo.

Yanga sc iliyopo kileleni mwa ligi kuu jioni ilifanya mazoezi yake katika uwanja wa Ccm Kirumba kuwasubiri Pamba Jiji siku ya mchezo huo.

Ikiwa kileleni mwa ligi kuu Yanga sc inapaswa kushinda mchezo huo ili kuendelea kuongoza msimamo hasa baada ya sare ya 2-2 iliyopata Simba sc dhidi ya Azam Fc siku ya jumatatu.

Nao Pamba Jiji sio wanyonge tangu duru la pili la ligi kuu lianze baada ya kuwa na michezo mizuri wakiwafunga Azam Fc katika uwanja huo wa Ccm Kirumba na mpaka sasa wana alama 22 katika michezo 21 ya ligi kuu wakiwa katika nafasi ya 12 ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala