Connect with us

Makala

Yanga sc Yavuna Mamilioni ya Wananchi

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuvuna kiasi kikubwa cha pesa katika tamasha la wiki ya mwananchi baada ya kuvuna zaidi ya Tsh 520 milioni kutokana na viingilio.

Katika siku hiyo ya kilele ambapo mgeni rasmi alikua ni kocha bora barani Afrika Pitso Mosimame licha ya kupoteza mchezo huo 2-0 dhidi ya Vipers Fc mabosi wa klabu hiyo wanachekelea mapesa mengi waliyovuna kutokana na viingilio ambapo kiingilio cha chini ilikua ni Tsh.10000 huku cha juu kikiwa ni Tsh.300,000/=.

Katika viti vya mzunguko ambapo waliweka kiingilio cha shilingi elfu kumi walivuna kiasi cha milioni 375 na ushee huku Vip A wakivuna milioni 20 na Vip B wakivuna milioni 102 na chenji kadhaa huku Vip C wakivuna milioni 23 na kufanya jumla kuu kuwa 521,460,000 huku Tofauti na watani wao wa jadi Simba sc ambao katika tamasha lao la Simba day wakivuna takribani milioni 313 pekee.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala