Connect with us

Makala

Manzoki,Lwanga Kuwavaa Yanga sc

Klabu ya Yanga sc kesho inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Vipers Fc katika kuadhimisha tamasha la wiki ya mwananchi ambalo hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa msimu mpya wa ligi kuu nchini.

Katika Tamasha la mwaka huu Yanga sc itamenyana na mabingwa wa ligi kuu nchini Uganda Vipers Fc ambao wamekuja na mshambuliaji anayewaniwa na klabu ya Simba sc Cezar Manzoki mfungaji bora na mchezaji bora wa ligi ya Uganda msimu uliopita.

Mbali na Manzoki ambaye klabu yake imewataka Simba sc kama wanamhitaji kupeleka ofa yao mezani wakigoma na kukanusha kuwa anakaribia kumaliza mkataba wake pia Thaddeo Lwanga ambaye ametemwa na Simba sc amejiunga na klabu hiyo na atashiriki mchezo huo hapo kesho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala