Connect with us

Makala

Yanga sc Yatinga Fainali Cafcc

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho nchini baada ya kuifunga klabu ya Marumo Gallants ya nchini Afrika ya kusini kwa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Afrika Kusini katika uwanja wa Royal Bafokeng ulioko katika mji Rustenburg.

Yanga sc iliingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya goli mbili ilizopata hapa nchini na ilianza na kikosi chenye walinzi wanne huku watatu kati yao wakiwa ni walinzi wa kati wakiongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto huku eneo la ushambuliaji wakiamuanzisha Fiston Mayele na Kennedy Musonda na Mudathir Yahya akianza katika nafasi ya Stephane Aziz Ki.

Marumo hawana budi kujilaumu wenyewe kutokana na kukosa nafasi kadhaa za wazi kipindi cha kwanza mpaka pale dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza ambapo Mayele aliwazidi mbio walinzi wa Gallants na kufunga bao la uongozi.

Kipindi cha pili Gallants walikuja na akili ya kushambulia huku wakiacha nafasi kubwa eneo la ulinzi na kuwafanya Yanga sc kupata nafasi kadhaa za kufunga huku Mudathir Yahya alikosa umakini kumalizia nafasi hizo ambapo Mayele tena dakika ya 62 alimzidi mbio mlinzi wa kati wa Gallants na kutoa pasi kwa Musonda aliyefunga bao la pili kwa Yanga sc.

Kuingia kwa bao hilo kuliwachanganya wenyeji ambao walipoteza umakini na kujikuta wakikoswakoswa magoli mengine kadhaa huku mwalimu Nabi akiwaingiza Jesus Moloko,Aziz Ki na Clement Mzize.

Ranga Chivaviro alionyesha umakini wake akifunga bao la sita katika michuaano hiyo akiwazidi maarifa kipa Djigui Diara na Bakari Mwamnyeto dakika ya 90+4 na mpaka mpira unamalizika matokeo yalikua 2-1 na Yanga sc kufuzu fainali ambapo atakutana na Usm Algers ya nchini Algeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala