Connect with us

Makala

Yanga Sc Yarejea Kileleni Ligi Kuu

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga timu ya Kmc Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.

Ikitoka kupata suluhu dhidi ya Jkt Tanzania katika mchezo uliopita,Yanga sc ilianza mchezo kwa kasi ikishambulia ambapo mastaa Mudathir Yahaya,Clement Mzize na Stephan Aziz Ki walikosa nafasi za wazi za mabao.

Krosi ya Maxi Nzengeli iliunganishwa kwa kichwa na Prince Dube na kuipatia Yanga sc bao la uongozi dakika ya 10 ya mchezo huo huku Stephane Aziz Ki akifunga kwa penati baada ya Mzize kuangushwa ndani ya boxi la Kmc dakika ya 18.

Ki alifunga tena mabao mawili mengine dakika za nyongeza na dakika ya 56 ya kipindi cha pili kwa penati baada ya Prince Dube kuangushwa akielekea kufunga.

Mabadiliko ya mwalimu Hamdi Miloud kuwaingiza Pacome Zouzoua,Cletous Chama na Abubakar Salum yalileta uhai kwa Yanga sc ambapo waliishambulia Kmc muda wote.

Maxi Nzengeli alifunga bao la tano kwa Yanga sc dakika ya 90 akipokea pasi nzuri ya Prince Dube huku Israel Mwenda akifunga bao la sita kwa pasi ya Dube kwa mara nyingine dakika za nyongeza za mchezo huo.

Yanga sc sasa imerejea kileleni ikiwa na alama 49 katika michezo 19 ya ligi kuu ikiitangulia Simba sc mchezo mmoja yenye alama 47.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala