Connect with us

Makala

Yanga sc Yakusanya 1Bn

Klabu ya Yanga sc kupitia mchakato wake wa usajili wa wanachama wa klabu hiyo umetangaza kukusanya kiasi cha zaidi Shilingi Bilioni moja za kitanzania kupitia mchakato wake wa usajili wa wanachama kwa njia za kidigitali ambao unafanyika kwa ushirikiano na kampuni ya Kilinet Africa.

Mfanikio hayo iliyoyapata klabu hiyo ni ndani ya kipindi cha miezi sita pekee ambapo imefanikiwa kusajili wanachama 34,650 na kukusanya mapato ya Tshs Bilioni 1.07 kwa mujibu wa taarifa kutoka klabuni hapo ambayo ilitolewa mchana wa leo katika mkutano na waandishi wa habari.

Mohammed Kirra Mtendaji Mkuu wa Kilinet alisema kuwa “Tumekuwa tukisafiri mikoa mbalimbali na takwimu zinaonyesha katika mkoa ambao umeongoza kwa usajili wa idadi kubwa ya wanachama ni Dar es Salaam ambao tulisajili wanachama 12124,”.

“Kwa upande wa Kanda takwimu zetu zinaonyesha kwamba Pwani ndio imeongoza kwa kutupatia wanachama 15,804.huku akimalizia kusema kuwa kuwa baada ya mafanikio hayo ya eneo la usajili wa wanachama sasa wataingia katika sura nyingine ya usajili wa mashabiki ambao watakuwa wakilipa kiasi cha sh 17,000 kwa ada ya mwaka.

Yanga sc kwa kushirikiana na kampuni hiyo imekua ikizunguka nchini nzima kwa lengo la kusajili wanachama wake katika mfumo rasmi ili watambulike na waweze kuingizia mapato klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala