Connect with us

Makala

Yanga Sc Yaipa Kipigo Heavy Kengold Fc

Klabu ya Yanga sc imeweka historia ya kufunga mabao mengi katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini msimu huu baada ya kuifunga Kengold Fc 6-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Ikiwa chini ya kocha msaidizi Abdulhamid Moalin Yanga sc ilianza kupata bao la mapema dakika 2 likifungwa na Prince Dube huku dakika ya sita ikipata bao la pili kupitia kwa Clement Mzize na kisha Pacome Zouzoua alifunga bao la tatu ambalo baada ya dakika 4 Mzize tena akafunga bao la nne ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Dakika ya 46 ya mchezo Dube akafunga bao la pili kwake na la tano kwa Yanga sc kwa kichwa akiunganisha pasi nzuri ya Chadrack Boka baada ya mabeki wa Kengold Fc kujisahau kuokoa mpira wa krosi hiyo.

Duke Abuya aliyechukua nafasi ya Khalid Aucho alifunga bao la sita kwa Yanga Sc dakika ya 85 akimalizia pasi ya Kennedy Musonda lakini dakika moja mbele Selemani Bwenzi alimtungua kipa Djigui Diarra kwa shuti la mbali na kuipatia Kengold Fc bao la kufutia machozi.

Yanga sc baada ya ushindi huo sasa imefikisha alama 45 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini huku Simba sc ikiwa nafasi ya pili ambapo kesho itavaana na Fountain Gate Fc.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala