Connect with us

Makala

Yanga sc Yaimaliza Kmc

Ikianza na kikosi cha wachezaji wengi ambao wanaanzia benchi Yanga sc imefanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kmc uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc ilipata bao hilo dakika ya 38 kupitia kwa Clement Mzize aliyeunganisha mpira uliotemwa na kipa David Kissu Mapigano aliyeshindwa kuokoa mpira wa kona na kumkuta mfungaji huyo kinda aliyeanza badala ya Fiston Mayele.

Mzize aliyesaidia na Stephane Aziz Ki sambamba na Dickson Ambundo na Tuisila Kisinda alikosa mabao kadhaa ya wazi kutokana na kukosa utulivu katika eneo hilo la mbele.

Kmc licha ya kujitahidi kusawazisha bao hilo milango ilikua migumu upande wao kutokana na uwezo wa kipa Djigui Diarra katika kuwapanga mabeki wake wakiongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto aliyecheza pacha na Ibrahim Abdalah Bacca.

Yanga sc sasa imefikisha alama 62 katika michezo 23 ya ligi kuu ikiiwaacha Simba sc kwa alama nane huku zikiwa zimesalia mechi saba kwa kila timu kumaliza msimu wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala