Connect with us

Makala

Yanga sc Yaiadhibu Mbeya Kwanza

Baada ya Dodoma Jiji Fc sasa ilikua ni zamu ya Mbeya kwanza Fc kupata adhabu baada ya kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Mbeya kwanza waliingia na staili ya kujilinda zaidi ambapo idadi kubwa ya wachezaji ilibaki nyuma ya mstari wa katikati ya uwanja huku wakiwaacha Eliuta Mpepo na Habib Kiyombo wakiwa hawana msaada/

Fiston Mayele kwa mara ya kwanza alitetema baada ya kutofunga kwa michezo minne ya ligi kuu ambapo alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Salum Abubakari ‘Sure Boy’ dakika ya 34 huku Dakika tano baadae pasi ya Khalid Aucho ilimkuta Saido Ntibanzokiza ambaye alimchungulia kipa na kufunga bao la pili na la saba kwake.

Ikiwa zimesalia dakika tatu za nyongeza Dickson Ambundo alimalizia kazi nzuri ya Jesus Moloko akifunga dakika ya 45 ya mchezo na kufanya Yanga sc kwenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 3-0.

Yanga sc ilifanya mabadiliko ikiwa zimesalia takribani dakika 30 mchezo kumalizika ikiwatoa Fiston Mayele,Jesus Moloko,Dickson Ambundo na nafasi zao kuchukuliwa na Chico Ushindi,Heritier Makambo na Chrispine Ngushi ambapo Makambo alifunga bao la kwanza la ligi kuu msimu huu dakika ya 74 huku akikosa nafasi kadhaa za wazi.

Dakika 90 zilimalizika kwa Yanga sc kuondoka na alama tatu na kufikisha jumla ya alama 63 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini wakiwa wamecheza jumla ya michezo 25 ya ligi kuu huku Mbeya kwanza wakiwa mwishoni na alama 21 katika hatari ya kushuka daraja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala