Connect with us

Makala

Yanga sc Yabanwa Kigoma

Klabu ya Yanga sc imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting uliofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu.

Yanga sc haina budi kumshukuru mshika kibendera ambaye alikataa goli la Ruvu Shooting akidai kuwa mfungaji alikua ameotea na kuwafanya Yanga sc waendelee kubaki mchezoni mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika mchezo ulikua suluhu huku Ruvu Shooting wakishukuru baada ya Fiston Mayele kugongesha mwamba mara mbili akijaribu kumfunga golikipa Mohamed Makaka.

Kutokana na msimamo huo Yanga sc anafikisha alama 56 huku akifuatiwa na Simba sc yenye alama 43 ikiwa na mchezo mmoja mkononi huku Ruvu Shooting ikiwa katika nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 22.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala