Connect with us

Makala

Yanga sc Wazindua Kadi za Kielektroniki

Klabu ya Yanga sc imezindua rasmi zoezi la ugawaji wa kadi za elektroniki za mashabiki na wanachama wa klabu hiyo leo jijini Dodoma katika hafla iliyofanyika Morena Hoteli huku mgeni rasmi akiwa spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Tulia Akson.

Katika hafla hiyo wabunge ambao ni mashabiki na wanachama wa klabu hiyo walipatiwa kadi hizo huku wanachama na mashabiki wa kawaida wakitakiwa kukamilisha usajili kupitia matawi yao ili waweze kuzipata kadi hizo.

Kadi hizo zina faida mbalimbali ikiwemo kufanyia manunuzi mengine pamoja na kukatia tiketi ya kuingia uwanjani huku ikiwa inatengenezwa na kampuni ya N-Card.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala