Connect with us

Makala

Yanga sc Watua Dodoma Kibabe

Kikosi cha klabu ya Yanga sc kimewasili jijini Dodoma kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Nbc dhidi ya Dodoma jiji siku ya Jumapili utakaofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini humo.

Yanga sc itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuwafunga walima zabibu hao kwa magoli 4-1 katika mchezo wa awali jijini Dar es salaam ambapo pia watahitaji kuongeza alama katika mbio za ubingwa wa ligi hiyo.

Yanga sc imefikisha jumla ya michezo mitatu bila ushindi japo imeendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 57 katika michezo 23 huku presha ya ubingwa ikitajwa kama chanzo cha kupata matokeo hayo.

Mchezo huo awali ulikua uchezwe saa moja usiku lakini kutokana na uwanja kuwa na matumizi mengine hivi sasa utachezwa saa 1o jioni katika uwanja huo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala