Connect with us

Makala

Yanga Sc Vs Singida Black Stars Kmc Leo

Ni kivumbi leo katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam ambapo miamba miwili ya ligi kuu Yanga sc itavaana na Singida Black Stars jioni ya leo katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

Yanga sc itaingia katika mchezo huo ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 49 huku pia ikishinda mchezo wake uliopita dhidi ya Kmc kwa mabao 6-1 huku Singida Black Stars yenyewe ikiwa nafasi ya nne ya msimamo ikiwa na alama 39 katika msimamo wa ligi ya Nbc.

Kocha wa klabu ya Yanga sc Hamdi Miloud amesisitiza kuwa ataingia katika mchezo huo kwa staili ile ile ya kushambulia huku akimheshimu mpinzani wake.

“Wanaonifahamu wanajua namna gani nina kuwa na uchu wa kupata ushindi, lakini hilo haliondoi ukweli kwamba tunapaswa kuwaheshimu wapinzani”,Alisema Miloud

“Nikisema nawaheshimu wapinzani haimaanishi nina hofu, namaanisha mpira ni mchezo wa ushindani na kila mtu anatumia mbinu mbalimbali kujaribu kushinda hivyo lazima niende kwa tahadhari na umakini hata kama nahitaji kupata alama tatu”,Alimalizia kusema Miloud Hamdi ambaye amejiunga na Yanga Sc akitokea Singida Black Stars

David Ouma ambaye ni Kocha wa Singida Black Stars alisisitiza kuwa yeye ataingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa.

“Nafahamu ubora wa mpinzani wangu hivyo nitajiandaa kuvaana nae kwa tahadhari kubwa ili kuweza kupata alama tatu muhimu”.Alisema Ouma aliyewahi kuwa kocha wa Coastal Union.

Mchezo huo unatarajiwa kutoa muelekeo wa mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini ambapo endapo Yanga sc itafanikiwa kushinda basi itazidi kuongeza wigo wa alama za kuongoza ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala