Tambo mbalimbali za makocha na wachezaji wa klabu za Yanga sc na Azam Fc zimeendelea kuhamasisha mchezo huo utakaopigwa kesho katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
Mapema hii leo katika mkutano na waandishi wa Habari kocha Miloud Hamd alisema kuwa kikosi chake kimejiandaa vyema kuelekea mchezo huo huku akisisitiza kuwa anafahamu ubora wa kikosi cha Azam Fc.
“Tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC, hautakuwa mchezo rahisi lakini mchezo muhimu na wa aina hii ndiyo mchezo ambao tunatakiwa kuhakikisha tunacheza kwa umakini na kupata ushindi” Alisema kocha Miloud Hamdi mbele ya waandishi wa Habari.

Naye mlindi Dickson Job alisema kuwa wao kama wachezaji wamejiandaa vyema kabisa kufuata maelekezo ya mwalimu katika mchezo huo huku akisema kuwa anatambua kama Azam Fc ni timu bora na mchezo huo utakua mgumu huku akiahidi ushindi.
“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu hatuna kitu kingine cha kuwaahidi mashabiki wetu zaidi ya kwenda kupambana jasho na damu kuhakikisha tunapata ushindi, maandalizi ni mazuri na wote tunafahamu umuhimu wa mechi ya kesho” Dickson Job
Naye kocha wa Azam Fc Rachid Taoussi alisema kuwa wao wanatambua ubora wa Yanga sc na wamejipanga kuwadhibiti ili kuchukua alama tatu muhimu baada ya kupoteza dhidi ya Singida black stars.
“Tunatambua tunakwenda kukutana na timu ya namna gani na ubora wao uko wapi hivyo tutapambana kupata alama tatu baada ya kuzikosa katika mchezo uliopita”Alisema Taoussi
Mchezo baina ya vilabu hivyo siku za hivi karibuni umekua na upinzani mkali kutokan ana ubora wa timu zote mbili ambapo katika mchezo wa awali Azam Fc iliibuka na ushindi wa bao 1-0.