Connect with us

Makala

Yanga sc Kimataifa Ikiwa Kileleni

Ushindi wa 2-0 ilioupata klabu ya Yanga sc dhidi ya Namungo Fc umeifanya klabu hiyo kurejea katika michuano ya kimataifa ikiwa kileleni mwa ligi kuu nchini ambapo imefanikiwa kuwa na alama 59 mpaka sasa katika michezo 22 ya ligi kuu mpaka sasa huku ikiwa imesaliwa na michezo minane tu ambapo ikishinda sita inaweza kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu nchini msimu wa 2022/23.

Yanga sc katika mchezo huo iliingia kwa kujiamini ikipanga mashambulizi kwa umakini mkubwa hasa katika safu ya kiungo iliyokua na Mudathir Yahaya na Khalid Aucho lakini changamoto ya mawinga Moloko na Farid kutokua na kiwango bora kulisababisha timu hiyo kukosa magoli kutokana na mawinga hao kushindwa kumlisha Fiston Mayele.

Dickson Job alifunga kwa kichwa bao la uongozi dakika ya 43 huku makosa binafsi ya kipa Deo Munishi yakimpatia Stephan Aziz Ki bao la pili kwa Yanga sc ambao kama wangekua makini wangefunga zaidi ya bao tatu hasa baada ya Mayele kukosa mabao ya wazi.

Timu hiyo sasa itaelekea katika michuano ya kimataifa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho dhidi ya Us Monastry katika mchezo utakaofanyika nchini Tunisia siku ya Jumapili Februari 12 na baada ya hapo itarejea nchini kuwasubiri Tp mazembe katika uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 19.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala