Connect with us

Makala

Yacouba Kukiwasha Mapinduzi Cup

Mshambuliaji wa Yanga Yacouba songne ataanza kuwatumikia Wananchi kwenye mashindano ya mapinduzi cup visiwani Zanzibar yanayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi January mwakani visiwani Zanzibar.

Kocha mkuu wa Yanga Professor Mohamed Nasreddine Nabi amepanga kumpa nafasi ya kutosha Yacouba songne kwenye mashindano ya hayo kabla hajamrudisha rasmi kwenye kikosi ambacho kinacheza mashindano yote ya ndani na nje huku ikitarajiwa kwamba anaweza kuchukua nafasi ya staa mmoja wa kigeni kikosini humo.

Pia inasemekana kwamba Professor Mohamed Nasreddine Nabi amepanga kuyatumia mashindano ya kombe la mapinduzi Kama sehemu ya kuiandaa timu kabla ya kuanza michezo ya kimataifa kwenye ngazi ya makundi ambapo Yanga sc wamepangwa katika kundi D na Timu za Tp Mazembe,Real Bamako na El Monastry ya nchini Hispania.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala