Connect with us

Makala

Simba sc Wampiga 5G Geita Gold sc

Klabu ya Simba sc imefnikiwa kuibuka na alama tatu baada ya kumfunga Geita Gold Sc mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Iliwachukua Simba sc dakika 12 kupata bao la kwanza ambapo John Bocco aliunganisha krosi ya Shomari Kapombe huku Cletous Chama akifunga bao la pili dakika ya 40 akitumia ujanja binafsi na kuwaacha mabeki wakiwa hawana ujanja huku Pape Osmane Sakho akifunga bao la tatu dakika ya 47 kwa shuti kali.

Sakho alifunga tena dakika ya 75 akimchungulia kipa ambaye alikua ametoka golini huku pia Chama akimpasia Kibu Dennis na mpaka matokeo yanaisha Simba sc ilimaliza na mabao 5-0 na kufanikiwa kupaa katika nafasi ya pili ikiwa na alama 37 katika msimamo wa ligi kuu nchini huku ikiwa imecheza jumla ya michezo 16.

Simba sc sasa itavaana na Kagera Sugar katika mchezo unaofata utakaofanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambapo mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala