Connect with us

Makala

‘Wananikamia Sana’Mayele Afunguka Kutofunga

Staa wa klabu ya Yanga sc Fiston Mayele amefunguka sababu ya kutofunga bao lolote katika mechi nne za ligi kuu ni kutokana na mabeki kumkamia sana ili asifunge na kushangilia kwa staili yake ya kutetema.

Mayele alisema hayo wakati wa mahojiano na vyombo vya habari baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Dodoma jiji Fc ambapo amefikisha jumla ya mechi nne akiwa hajafunga bao lolote kuanzia mechi ya Simba sc,Ruvu shooting,Tanzania Prisons na Dodoma Jiji ambapo Yanga sc ilishinda kwa mabao mawili ya Dickson Ambundo na kipa Yussufu Mohamed wa Dodoma jiji akijifunga.

‘wananikamia sana mabeki ili nisiteteme lakini mashabiki wasiwe na wasiwasi malengo ya timu kwanza na ya kwangu yanafuatia’Alisema Mayele mwenye mabao 12 ya ligi kuu msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala