Connect with us

Makala

Utata Wazuka Simba Sc Vs pamba Jiji

Presha ya mchezo wa ligi kuu baina ya klabu za Pamba Jiji dhidi ya Simba Sc utakaofanyika jioni ya leo imezidi kuwa juu baada ya kutokea mvutano wakati wa mazoezi ya mwisho ya klabu ya Simba Sc katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Simba sc wakiwa katika mazoezi ya mwisho katika uwanja huo utakaofanyika mchezo huo kwa mujibu wa Kanuni za ligi kuu nchini hawakupaswa kuingiliwa na watu wa aina yeyote lakini uwepo wa baadhi ya maafisa wa Pamba Jiji katika chumba cha mikutano ilileta sintofahamu baina ya pande mbili.

Hali hiyo ilizua ghasia ambazo zilisababisha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza chini ya Mwenyekiti Mh.Said Mtanda ambaye ni mkuu wa mkoa huo kufika na kuwakamata baadhi ya viongozi wa Simba sc akiwemo kocha msaidizi Selemani Matola na Meneja Patrick Rweyemamu.

Tayari watu hao walishaachiwa jana usiku huku Simba sc wakitoa taarifa kulaani suala hilo na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza na yenyewe ikitoa ufafanuzi wa kina ambapo walidai kuwa walikua katika shughuli za kawaida kuhakikisha ulinzi na usalama kuelekea mchezo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala