Connect with us

Makala

Tambwe Atemwa Singida Big stars.

Klabu ya Singida Big Stars iko mbioni kumalizana na mshambuliaji Amis Tambwe kwa lengo la kuvunja mkataba baada ya kutoridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo aliyeisaidia timu hiyo katika kupanda daraja.

Tambwe mchezaji wa zamani wa Yanga sc amekosa nafasi mbele ya mastaa wenzie Meddie Kagere na Fancy Kazadi ambao kocha Hans Van de Pluijm amekua akiwatumia mara kwa mara kama washambuliaji wake kikosini humo.

“Tambwe pia hataweza kucheza msimu ujao, alitakiwa kuondoka tangu dirisha dogo lakini makubaliano hayakwenda vizuri kama tulivyokuwa tunatarajia.” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake litajwe hadharani.

Pamoja na Tambwe pia walima alizeti hao wapo mbioni kuachana na mchezaji raia wa Brazil Dario Federico baada ya benchi la ufundi kuamua kuachana nae huku wakijiandaa kusajili beki mmoja na mshambuliaji mmoja kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala