Connect with us

Makala

Tabora United Kuvuna 50m Kisa Simba Sc

Klabu ya Tabora United imeahidiwa kupata zawadi ya shilingi milioni hamsini za kitanzania endapo itaifunga klabu ya Simba Sc katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika Februari mosi mwaka huu.

Awali mchezo huo ulisogezwa mbele kutokana na Simba sc kukabiliwa na michuano ya Kimataifa mna sasa bodi ya ligi kuu baada ya kuahirishwa kwa fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) sasa imetangaza ligi kuu kurejea mwanzoni mwa mwezi ujao kwa michezo ya viporo.

Tabora United ilishawafunga Yanga sc pamoja na Azam Fc na kuzoa alama sita kwa timu hizo kubwa nchini.

“Mie namshangaa sana Ahmed anakuwa muoga muoga, mtoto wa kiume hutakiwi kuwa muoga nilazima ukabiliane na tatizo ambalo utakutana nalo”,Alisema Christina Mwagala mkuu wa idara ya habari ya klabu hiyo.

“Inshu ya Bonus ndio naona watu wanaikuza kuza ila sisi bonus tumeanza kupewa tangu tumeanza Msimu na mkuu wetu wa Mkoa, Timu ikitoa sare ni milioni 5, ikishinda ni milioni 10”,Aliendelea kusema.

“Lakini kuelekea mchezo dhidi ya Simba amewiwa kutuongezea dau la milioni 50, kwahiyo imekuwa kawaida yetu kula na kunywa na mkuu wetu wa Mkoa wa Tabora”, Alimalizia Christina Mwagala Afisa habari wa Club ya Tabora United akielezea kwa kina kuhusu suala hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala