Connect with us

Makala

Sven Akanusha Taarifa Za Mitandaoni

Kocha mkuu wa Simba Sc,Sven Vandenbroeck amekanusha taarifa zilizoenea mtandaoni kuhusu nyota wake namba moja Meddie Kagere kuwa walipigana.

Sven amesema kuwa taarifa hizo si za kweli na hawezi kutumia nguvu kulizungumzia hilo kwakuwa halina maana kwani hajui wapi lilipotokea hadi kuzuka mitandaoni.

“Ninaloweza kusema ni kuwa sina tatizo na Meddie Kagere”alisema Sven baada yakutotaka mahojiano marefu.

Sven ameshaanza kazi ya kukinoa kikosi chake cha Simba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu bara msimu wa 2020/2021 unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya dhidi ya Ihefu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala