Connect with us

Makala

Stars,Sudan Watoshana Nguvu

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kutoka sare ya 1-1 na timu ya Taifa ya Sudan katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya Fifa uliofanyika nchini Saudi Arabia siku ya Jumapili Oktoba 15.

Mchezo huo ulilazimika kufanyika nchini humo kutokana na hali hafifu ya usalama inayoendelea nchini Sudan hivyo kuwalazimu wenyeji kutafuta uwanja huru.

Ikianza na mfumo wa 3-4-3 golini akisimama kipa Beno Kakolanya huku Ibrahim Hamad,Dickson Job na Bakari Nondo wakiwa kama mabeki wa kati na Haji Mnoga,Novatus Dismas,Mzamiru Yassin na Sospeter Bajana wakiwa kama wachezaji wa eneo la kiungo huku Simon Msuva,Mbwana Samata na George Mpole wakicheza eneo la ushambuliaji.

Stars iliruhusu bao la mapema dakika ya 7 ya mchezo ambapo kablaya kipindi cha kwanza kuisha Stars walisawazisha kupitia kwa Sospeter Bajana kwa shuti kali dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza.

Stars inayonolewa na kocha Adel Amrouche imeamarika kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kufanikiwa kufuzu michuano mikubwa ya mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani mwezi januari nchini Ivory Coast.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala