Connect with us

Makala

Stars,Afcon Kimeumana

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) usiku wa leo itafahamu wapinzani wake watatu katika kundi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast ambapo  droo itakayochezeshwa Abidjan itaamua nani na nani watakakutaana katika michuano hiyo.

Kwenye droo hiyo itakayofanyika majira ya saa tatu usiku itakayoongozwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania itakuwa katika chungu cha nne pamoja na Guinea Bissau, Msumbiji, Namibia, Angola na Gambia.

Kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa na CAF uchezeshaji wa droo hiyo kutakuwa na makundi sita yatakayoundwa na timu nne, moja kutoka kila chungu kati ya vinne vitakavyokuwa na timu sita kila kimoja kulingana na nafasi ambayo ipo katika viwango vya ubora.

Timu mwenyeji, Ivory Coat itapangwa kundi A na hivyo atasubiri nyingine tatu kutoka katika chungu namba mbili, tatu na nne.

Kitendo cha Tanzania kuwekwa katika chungu cha nne kinaiweka katika uwezekano wa kupangwa kundi gumu kutokana na ubora wa vikosi na wachezaji wa timu zilizopo katika vyungu vitatu tofauti na ambacho Taifa Stars ipo.

Ikumbukwe hii mara ya tatu kwa Taifa Stars kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za timu ya Taifa barani Afrika ambapo walishiriki mwaka 1980,2019 na mwakani 2024.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala