Connect with us

Makala

Stars Yang’ara

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Afrika ya kati katika mchezo wa kirafiki wa kalenda ya Fifa uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Stars ilianza na kikosi cha vijana ikiwajumuisha Metacha Mnata,Haji Mnoga,Nickson Kibabage,Dickson Job,Bakari Mwamnyeto,Novatus Dismas,Feisal Salum,Ben Starkie,Kelvin Joshua,Adi Yussuph na Mbwana Samata ambapo dakika 10 zilitosha kwa Stars kuandika bao la uongozi kupitia kwa Novatus Dismas aliyepiga faulo na mpira kumshinda golikipa ambapo mpaka mapumziko stars iliendelea kuongoza kwa bao hilo.

Kipindi cha pili Stars ilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Farid Mussa,Lusajo Mwaikenda ambapo mabadiliko hayo yaliinufaisha Taifa Stars ambayo ilipata bao la pili dakika ya 63 likifungwa na nahodha Mbwana Samata ambaye alipokea pasi murua kutoka kwa Farid Mussa ambaye alikua anacheza kama beki wa kushoto.

Kuumia kwa Novatus Dismas kulitoa nafasi kwa kiungo wa Mbeya City Aziz Andambwile kuingia na kufanikiwa kuonyesha soka safi lililowakonga nyoyo mashabiki ambapo Stars ilifanikiwa kufunga bao dakika ya 93 likifungwa na George Mpole na mpaka mpira unamalizika Stars iliibuka na ushindi huo mnono.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala