Connect with us

Makala

Sowah Aitamani Yanga Sc

Mshambuliaji wa klabu ya Singida Black Stars Jonathan Sowah anatamani siku moja aitumikie klabu ya Yanga kwa sababu ya yale makubwa ambayo amefanyiwa na Rais wa Yanga Eng. Hersi Said.

Sowah aliyasema hayo mara baada ya kuisaidia klabu yake ya Singida Black Stars kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Jkt Tanzania siku ya Alhamis jioni.

Katika mchezo huo Sowah alipachika bao moja dakika ya 51 ya mchezo huo akipokea pasi nzuri ya Athur Bada na kuifanya Black Stars kufikisha alama 37 katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Sowah punde baada ya mchezo huo waandishi wa habari walimuuliza kuhusu kuichezea Yanga sc ndipo alipoamua kufunguka kwa undani zaidi.

“ Yanga ni nyumbani kwangu Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said ni kama Baba kwa yote aliyonifanyia. Naamini siku moja nitacheza Yanga kwa mafanikio zaidi”,Alisema Sowah.

Sowah amesajiliwa na Singida Black Stars katika dirisha dogo la usajili ya mwezi Januari mwaka huu na mpaka sasa ameichezea klabu hiyo mechi tatu za ligi kuu na kufunga mabao mawili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala