Connect with us

Makala

Singida FG Yatimua Kocha

Klabu ya Singida Fountain Gate Fc imetimua benchi la ufundi lililokua chini ya kocha Thabo Senong kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya klabuni hapo ambapo mpaka sasa kikosi hicho kipo katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu nchini kikiwa na alama 21 katika michezo 19.

Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo imsema kuwa kocha Senong pamoja na benchi lake la ufundi wakiwemo kocha wa Makipa,kocha msaidizi na kocha wa viungo wa klabu hiyo wametimuliwa ambapo sasa timu itakua chini ya kocha wa muda Ngawina Ngawina.

Kufanya vibaya kwa klabu hiyo kulianza baada ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili ambapo mastaa waliokua na msaada klabuni hapo walijiunga na Ihefu Fc ambapo mastaa kama Mauruf Tchakei,Dube Abuya,Morice Chukwu,Joash Onyango na kipa Abdalah Khomeiny ambapo wameisaidia Ihefu kuwa na matokeo mazuri siku za karibuni.

Taarifa za ndani pia zinadai klabu hiyo imekua na tatizo la kifedha ambapo baadhi ya mastaa wameanzisha mgomo baridi kushinikiza walipwe mishahara yao kwa wakati ambapo staa kama Bruno Gomez yeye ameamua kuvunja mkataba na klabu hiyo kutokana na hilo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala