Connect with us

Makala

Singida Black Stars Washangaa Miloud Kutua Yanga Sc

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kushtushwa na taarifa ya kocha wake Hamdi Miloud kujiunga na klabu ya Yanga sc kutokana na kuwa na mkataba naye.

Jana usiku klabu ya Yanga sc ilitangaza kuondoka kwa kocha Sead Ramovic na msaidizi wake huku ikimtangaza Miloud kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya klabu ya Singida Black Stars imesema kuwa uongozi wa klabu hiyo utachukua hatua ambapo kwa sasa imewaomba mashabiki kuwa watulivu wakati uongozi ukishughulikia suala hilo.

Miloud anaondoka klabuni hapo ambapo amezifundisha klabu ya Singida Black Stars kwa takribani mwezi mmoja pekee akisimama kama kocha mkuu katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Tma na Mbuni Fc ambazo zote aliibuka na ushindi.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala