Connect with us

Makala

Simba Sc Yatoa Dozi Cafcc

Klabu ya Simba Sc imeendelea kuuheshimisha uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Onze de Bravos ya Msumbiji.

Kocha Mkuu wa Simba sc Fadlu Davis aliamuanzisha nje mshambuliaji Lionel Ateba na kumuamini Steven Mukwala kuongoza jahazi aa Simba sc ambapo mikimbio na kasi ilikua silaha kubwa ya mchezaji huyo dhidi ya Bravos.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Jean Charles Ahoua kwa penati ambapo mpaka mapumziko matokeo yalibaki 1-0.

Kipindi cha pili Bravos waliamka na kusukuma mashambulizi ya kasi langoni mwa Simba sc ambapo kama si uimara wa kipa Mousa Pinpin Camara basi alama tatu za mchezo huo zilikua zipo rehani.

Mpaka dakika tisini za mchezo huo zinatamatika Matokeo yalibaki hivyo huku Simba sc ikikaa katika nafasi ya pili ya kundi A ambapo Cs Constantine wapo kileleni wakiwa na alama tatu kama Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala