Connect with us

Makala

Simba Sc Yatakata Moshi

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka alama tatu katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kuifunga mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.

Simba sc ikianza na safu ya ushambuliaji chini ya John Bocco na Moses Phiri ilifanikiwa kupata mabao hayo matatu yakifungwa na Bocco dakika ya 32 ya mchezo kisha Moses Phiri alifunga mabao mawili katika dakika za 43 na 53 na kufanikiwa kuumaliza mchezo mapema.

Polisi Tanzania walipata bao la kufutia machozi dakika za nyongeza na kufanya dakika 90 kumalizika kwa ushindi wa 3-1 kwa Simba sc na kupunguza presha za mashabiki wa klabu hiyo hasa baada ya kupata sare katika mchezo dhidi ya Mbeya City Fc.

Simba sc sasa imefikisha alama 31 katika michezo 14 ya ligi kuu huku ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini huku Yanga sc ikiongoza msimamo wa ligi kwa alama 32.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala