Connect with us

Makala

Simba Sc Yapigwa Faini TPLB

Klabu ya soka ya Simba, imetozwa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) kwa kosa la walinzi wake kuwazuia walinzi wa uwanjani (stewards) kumkamata shabiki aliyekuwa akitaka kuingia kiwanjani baada ya mchezo wao dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa Desemba 28, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) naye Kocha Robert Matano wa Fountain Gate FC, ametozwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kuwashutumu waamuzi waliochezesha mechi yao dhidi ya Simba SC iliyopigwa Februari 6, 2025.

Katika mchezo huo Simba sc ilipoteza alama moja baada ya kutoka sare ya 1-1 na Fountain Gate Fc kiasi cha kusababisha hali ya hewa kuchafuka katika mitandao ya kijamii.

Pamoja na hilo sasa tayari klabu hiyo imerejea kileleni mwa msimamo baada ya kuinyika Tanzania Prisons kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Kmc siku ya Jumatano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala