Connect with us

Makala

Simba sc Yapata Ceo

Klabu ya Simba sc imemtangaza Iman Kajula kuwa bosi mpya wa klabu hiyo kwa kipindi cha miezi sita ijayo akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez ambaye alijiuzuru nafasi hiyo hivi karibuni.

Kajuna ametangazwa leo kupitia vyanzo vya habari vya klabu hiyo ambapo atakua na jukumu la kusimamia uendeshaji na shughuli mbalimbali za klabu kama mtendaji mkuu wa klabu hiyo huku pia akihakikisha makombe yanarudi klabuni hapo kama ilivyokua hapo awali.

Kajuna ambaye kimsingi ni mwanachama na shabiki kindakindaki wa klabu hiyo anatajwa kuwa na uzoefu katika uongozi wa ngazi za juu akiwa bosi wa masoko na mawasiliano kwa nyakati mbalimbali katika benki za Crdb,Nmb na benki ya Posta huku pia kwa sasa akiwa ni mtendaji mkuu wa kampuni ya EAG Group.

Simba sc sasa itakua imeongozwa kwa ujumla na Watendaji wakuu watatu akianza Senzo Mazingisa kisha Barbara na sasa ni Iman Kajula.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala