Connect with us

Makala

Al Hilal Fc Yatua Nchini

Kikosi cha timu ya Al Hilal Fc ya nchini Sudan imetua nchini kuweka kambi ya siku kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mamelod Sundowns ya nchini Afrika ya kusini.

Ikiwa nchini katika kambi  hiyo ya siku kumi kikosi hicho kinachonolewa na kocha Frolent Ibenge kitacheza michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya Namungo Fc mchezo utakaochezwa Januari 26 kisha dhidi ya Azam Fc siku ya Januari 30 na Februari 5 siku chache kabla ya kikosi hicho kuondoka kitacheza dhidi ya Simba sc.

Baada ya michezo hiyo kikosi hicho kitaondoka nchini na kuelekea nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ikiwakilisha Kundi A dhidi Mamelod Sundowns siku ya Februari 11.

Baada ya mchezo huo timu hiyo itarejea nchini Sudan kuwasubiri Al Ahly siku ya Februari 18 kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi ikiwa ni michuano mikubwa kwa ngazi za vilabu barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala