Connect with us

Makala

Simba sc Yampeleka Manzoki China

Ni kama mchongo baada ya uongozi wa klabu ya Vipers Fc ya nchini Uganda kuamua kuwabania kuwauzia klabu ya Simba sc mchezaji Cezar Manzoki ambapo waliweka dau la zaidi ya milioni mia nne za kitanzania kwa Simba sc kuvunja mkataba wa miezi minne ya mshambuliaji huyo.

Vipers ilikua na lengo la kumsajili Manzoki katika mfumo wa usajili wa michuano ya kimataifa lakini staa huyo akashtuka na kuamua kujiunga na klabu ya Dallian Pro ya nchini humo kwa mkataba wa miezi minne ili arudi nchini mwezi novemba ama Desemba wakati wa dirisha dogo ili ajiunge na klabu yake anayoipenda ya Simba sc.

Manzoki ambaye alishinda tuzo tano katika ligi kuu ya Uganda msimu uliopita ikiwemo tuzo ya mfungaji bora ameonyesha nia ya dhahiri ya kujiunga na Simba sc ambapo mara kadhaa klabu hiyo imejaribu kuzungumza na Vipers Fc ambao wamekua wagumu kumuachia mchezaji huyo wakidai kuwa ana mkataba wa miaka miwili klabuni hapo japo mchezaji mwenyewe akisema mara kadhaa kuwa hautambui mkataba huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala