Connect with us

Makala

Azam Fc Yamtema Moallin

Klabu ya Azam Fc imeamua kuachana na kocha wake wa timu ya wakubwa Abdihamid Moallin pamoja na msaidizi wake Omary Nasser ambao wameachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi huku wakisubiri kupangiwa majukumu mengine ya kiufundi.

Maamuzi hayo yamefikiwa mapema kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu katika michezo miwili ya ligi kuu waliyocheza mpaka sasa ambapo katika michezo miwili wamefanikiwa kupata alama nne kati ya sita wakiwafunga Kagera Sugar 2-1 na kupaa sare dhidi ya Geita Gold ya 1-1.

Inasemekana kuwa mabosi wa klabu hiyo hawaridhishwi na ubora wa kikosi hicho ambapo wanaona kuwa kiwango cha timu kipo chini ukilinganisha na usajili waliofanya hivyo wanaona kama kocha hatoshi katika nafasi hiyo hivyo wanatafuta kocha mzoefu zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala