Connect with us

Makala

Simba sc Yaleta Mtaalamu wa Usajili

Klabu ya Simba sc imeazimia kuajiri mkurugenzi wa ufundi kwa ajili ya kusimamia mambo yote ya kiufundi ikiwemo usajili wa mastaa mbalimbali watakaoitumikia klabu hiyo tofauti na sasa ambapo usajili unafanywa na kamati maalumu ya usajili.

Simba sc imefikia kufanya hilo baada ya kusajili mastaa wengi ambao wameshindwa kuisaidia timu hiyo moja kwa moja hasa katika misimu hii miwili ya 2020/2021 na 2021/2022 ambapo klabu hiyo imemaliza bila kupata kombe lolote huku mafanikio pekee yakiwa ni kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Caf.

Simba sc ilimsajili Ismaël Sawadogo kipindi cha dirisha dogo lakini mchezaji huyo ameshindwa kuonyesha kiwango hali iliyopelekea mashabiki na wadau wa soka nchini kuzua mjadala kuhusu vigezo vilivyotumika kumsajili mchezaji huyo.

Inasemekana kuwa bosi wa klabu hiyo Mohamed Dewji ameridhia suala la kuajiriwa kwa mkurugenzi wa ufundi huyo huku kocha Roberto Oliveira ameruhusiwa kuamua nani aajiriwe katika nafasi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala