Connect with us

Makala

Simba Sc Yahamia New Amaan Complex

Klabu ya Simba Sc itautumia uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika siku ya Jumapili April 20 2025.

Simba sc katika mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali itakutana na timu ya Stelleboch Fc ya nchini Afrika ya kusini ambayo ilifanikiwa kuitoa Zamalek Fc ya nchini Misri.

Simba sc imelazimika kuhamia uwanjani hapo baada ya Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kuamua kuufungia uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na sehemu ya kuchezea kuharibika kutokana na mvua iliyonyesha kabla ya mchezo dhidi ya Al Masry Fc ambao Simba sc ilishinda kwa matuta 4-1.

Tayari kikosi hicho kimewasili Visiwani humo ambapo kitafanya mazoezi uwanjani hapo kwa siku tano ili kuzoea mazingira ya uwanja mpaka kufika siku ya mchezo April 20 ambayo itakua ni siku ya sikukuu ya Pasaka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala