Connect with us

Makala

Simba Sc Yaachana na Kennedy Juma

Ndoa baina ya beki Kennedy Juma na klabu ya Simba sc imefikia tamati rasmi hii leo baada ya klabu hiyo kutangaza kauchana na staa huyo mchana wa leo baada ya mkataba wake kufikia tamati.

Kennedy alisajiliwa na Simba sc mwaka 2019 akitokea timu ya Singida United ambapo sasa anaondoka kama mchezaji huru klabuni hapo kupisha usajili wa damu changa ambao utakuja kurudisha zama za mafanikio klabuni hapo.

Katika miaka yake mitano klabuni hapo Kennedy hawajawahi kuwa beki wa kutumainiwa ambapo mara nyingi alitumika kama chaguo la pili dhidi ya Pascal Wawa na Joash Onyango na msimu huu akisubiri kwa Henock Inonga na Che Fondoh Malone.

Taarifa za ndani zinadai kuwa klabu za Pamba Jiji,Kagera Sugar na Mashujaa United zinaonyesha nia ya kumsajili beki huyo mkongwe hapa nchini akiwa na uzoefu wa kucheza michuano ya ndani na ya kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala