Connect with us

Makala

Simba Sc Tayari Kuwavaa Singida Bss

Kikosi cha Timu ya Simba sc tayari kimekamilisha maandalizi yote muhimu kuwavaa timu ya Singida Black Stars katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika kesho Disemba 28 katika uwanja wa Liti mjini Singida.

Tayari kikosi hicho kimewasili mkoani humo tangu jana ambapo pamoja na kupata mapokezi makubwa leo jioni kimefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kasi zaidi ambao utatoa uelekeo wa Simba sc kuelekea mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini kutokana na timu hiyo kujaza mastaa wa maana nje ya timu za Simba sc,Yanga sc na Azam Fc.

Kocha Fadlu Davis amesisitiza umuhimu wa kupata alama tatu katika mchezo huo wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema siku ya leo.

“Tunahitaji kulinda kiwango chetu bora pamoja na kupata ushindi ambapo hayo ni mambo muhimu licha kutambua aina ya mshindani tunayekutana nae hivyo natambua mechi itakua na ushindani wa hali ya juu.

Pia kwa upande wa Kocha Ramadhan Nswazirumo yeye alisema atajitahidi kutumia kila aina ya silaha ili kupata ushindi.

“Ukiwa nyumbani unajua kila sila ilipo, unajua kisu kiko wapi, niseme tuna kila kitu ya kitufanya tushinde dhidi ya Simba.

“Htuchezi kwa mihemko, bali mipango kuounguza presha, kufungwa na Yanga, kufungwa na Azam hiyo imepita sasa tunacheza na Simba na tuko tayari kumfunga,”

Ramadhan Nswanzirumo, Kaimu Kocha Singida Blacks Stars.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Singida Black Stars imecheza michezo 15 mpaka sasa ikiwa nafasi ya nne ya msimamo ikivuna alama 33 huku Simba sc ikiwa kileleni na alama 37 katika michezo 14 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala