Connect with us

Makala

Simba sc Hali Si Shwari

Taarifa kutoka kwa baadhi ya wadau wa michezo zinasema kuwa mastaa wa klabu ya Simba sc wameweka mgomo baridi wakihitaji kumaliziwa posho zao za mechi nne wanazodai kwa uongozi wa klabu hiyo.

Mastaa hao wanadai posho za baadhi ya michezo kama ule wa Horoya Fc walioshinda 7-0 na michezo mingine kadhaa ya ligi kuu ya Nbc  huku katika mchezo dhidi ya Yanga sc wakiwa tayari wameshalipwa stahiki zao japo kulikua na makato ambayo mastaa hao hawajayaelewa vizuri.

Hilo limekuja kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Wydad Ac utakaofanyika siku ya Jumamosi ambapo lengo la mgomo huo ni kuushinikiza uongozi kumalizia madai yao haraka kabla ya mchezo huo.

Simba sc itakua na kibarua kigumu siku ya Jumamosi katika mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo wanapaswa kushinda mchezo huo kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala