Ni kufuru ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu ya Yanga sc kufanya shangwe la maana wakati wa hafla ya kushrekea ubingwa wa 28 wa ligi kuu nchini iliyofanyika wikiendi iliyopita jijini Dar es salaam wakati klabu hiyo iliporejea kutoka jijini Mbeya ambako ndipo ilipokabidhiwa kombe hilo.
Msafara wa magari na pikipiki pamoja na halaiki ya watu vilifika uwanja wa Taifa kuwapokea mastaa wa klabu hiyo wakiwa na kombe juu ya gari la kisasa maalumu kwa kusherekea makombe kama zofanyavyo klabu za ulaya kama Real Madrid na zinginezo ambapo walipitia barabara ya kutoka uwanja wa ndege wa J.kNyerere na kuingia mpaka kariakoo ambapo msafara ulipita mbele ya jengo la watani wao Simba sc kisha ukaelekea Jangwani ambapo kombe lilitambulishwa kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Baada ya utambulisho na dua klabuni hapo msafara ulielekea makao makuu ya wadhamini wa klabu hiyo mitaa ya Samora zilizopo kampuni ya Gsm ambapo ndipo kufuru ya bonge la pati ilifanyika huku wachezaji na viongozi wa klabu hiyo wakiserebuka na kula misosi ya maana wakiwa na baadhi ya mastaa ambao ni mashabiki wa klabu hiyo.
Kutokana na maandalizi na kufana kwa sherehe hizo vyombo mbalimbali vya habari za michezo vya kimataifa vimeipongeza klabu hiyo huku baadhi ya mastaa wengi akiwemo aliyekua kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane akipongeza shange hizo.